Mix

Alichokisema Shy-Rose Bhanji kuhusu jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Tanzania.

By

on

shyKatibu wa Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki Shy-Rose Bhanji amerejea Tanzania baada ya ziara ya siku 10 ya Wabunge wa EALA  nchini Kenya,karudi na la moyoni  kwa ajili ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hii ni  baada ya ziara yake ya siku 10 nchini Kenya ambayo ni ziara ya wabunge wa EALA iliyokua kwa mwaliko wa Serikali ya Kenya lengo likiwa kuhamasisha wananchi wa Kenya kupata ufahamu mkubwa juu ya Mtangamano wa Jumuiya na faida zake.

Shy Rose Bhanji anaelezea>>’Tulipata nafasi ya kuonana na Wananchi,Wafanyabiashara,Wabunge,Maseneta, Magavana,Asasi za kiraia na makundi mengine,ziara hii imenifungua macho zaidi kwamba bado tuna kazi kubwa mbele yetu kuhakikisha kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki inakuwa ni ya Wananchi (people Centred Integration)’

‘Kama nilivojionea mwenyewe kwa upande wa maeneo mbalimbali tuliyoyafikia bado mwamko wa ufahamu wa masuala ya EAC mdogo sana na kiu wa kuifahamu ni kubwa,hata hivyo Serikali ya Kenya kwa kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanashiriki kikamilifu juu ya masuala ya Jumuiya imefufua mpango huu wa wabunge wa EALA kufika Kenya kuendelea na zoezi la uhamasishaji’

‘Ni imani yangu kwamba na Serikali ya Tanzania itaiga mfano huu mzuri wa kuwaalika wabunge wa EALA kufika nchini ili kuwafikia makundi mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuhamasisha. Hata kwa upande wa Tz bado ufahamu wa wananchi wengi zaidi juu ya masuala ya Integration ni changamoto kubwa’

‘Lengo kuu la uanzishwaji wa EAC ni kuinua hali ya kiuchumi kwa wananchi wa Afrika Mashariki ambao sasa ni takriban millioni 140. Na iwapo mwamko wa wananchi ni mdogo basi lengo hili litachukua muda mrefu sana kufikiwa au kutokufikiwa kabisa’.

 

Tupia Comments