Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Askari Polisi wanawake kutoka Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kushiriki kikamilifu katika oparesheni zinazofanywa kwenye ukanda huo ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu.
Akifungua mafunzo ya siku Tatu ya Polisi wanawake kutoka SARPCCO katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam May 17, 2017 Makamu wa Rais amewahimiza Askari Polisi hao kufanya kazi kwa bidii na kujituma hatua itakayosaidia kupanda vyeo kama Askari Polisi wanaume katika maeneo yao ya kazi.
“Vyeo haviji tu ni lazima Polisi wanawake muonyeshe kuwa mnaweza ili muweze kupandishwa vyeo na kupata nafasi za uongozi katika Majeshi yenu.” – Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha, amesema kuwa kama Polisi wanawake wataacha majungu na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwao, watafikia malengo yao haraka hasa katika kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu ikiwemo biashara ya dawa za kulevya.
“Ukombozi wowote una vita, vita hii isituumize” – Nape