Ni headlines baada ya headlines inawezekana ulikuwa na maswali mengi kuhusiana na kauli ya tume ya Uchaguzi kuhusu kusimama mita 200 pale unapomaliza kupiga kura siku ya tarehe 25, 2015.
Sasa taarifa niliyoipata leo Octoba 20,2015 ni kwamba Mahakama Kuu ya Dar es Salaam kesho itatoa uamuzi wa Shauri linalohusu umbali wanaotakiwa kusimama wapiga kura siku ya Uchaguzi Mkuu Tanzania.
Jopo la majaji limeagiza upande wa mlalamikaji unaowakilishwa na mawakili Peter Kibatala na Omary Msemwa kubadili hati ya mashtaka na kumshtaki Mkurugenzi wa Uchaguzi badala ya Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi, kesi hiyo imevuta hisia za watu wengi kutokana na suala la tafsiri kuonekana kama kikwazo kwa vyama vinavyounda umoja wa katiba yaani UKAWA.
MillardAyoUPDATES: Mahakama Kuu Dar kesho itatoa uamuzi wa Shauri linalohusu umbali wanaotakiwa kusimama Wapigakura siku ya Uchaguzi Mkuu TZ
— millard ayo (@millardayo) October 20, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE