Mix

Sikukuu ya Mapinduzi bure huduma ya afya

on

Hospitali ya Elidad ya Boko Basihaya jijini Dar es salaam itaadhimisha sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar January 12 2021 kwa kufanya vipimo vya afya bure kupitia kampeni ya Afya Bure.

Mkurugenzi Mtendaji wa hospiatli hiyo DR Harry Matoyo alisema kuwa zoezi hili litafanyika Jumanne ijayo hospitalini hapo na siku hiyo watafanya uchunguzi wa magonjwa tofauti na kuwapa matibabu ya awali.

DR Matoyo alisema kuwa zoezi hilo litafanyika kuanzia asubuhi na watafanya uchuguzi wa magonjwa ya mifupa na viungo, uchunguzi wa magonjwa ya moyo na uchunguzi wa magonjwa wa kisukari.

Alisema kuwa wameamua kuadhimisha sikukuu hiyo kwa kutoa huduma bure ili kuunga mkono jitihada za Rais DR John Magufuli za kuondoa adui maradhi ambayo serikali haitaweza kufanya peke yake.

“Kuona kuwa serikali inapambana na adau maradhi, hospitali ya Elidad iliamua kuunga mkono serikali kwa kuanzisha Afya Bure Kampeni kwa lengo la kupambana na adui maradhi na kulijenga taifa lenye raia wenye afya njema”

Soma na hizi

Tupia Comments