Mwimbaji na mjasiriamali maarufu Oluwatosin Oluwole Ajibade almaarufu Mr Eazi amefichua kuwa hakuwahi kutaka kuwa mwanamuziki.
Alisema alifikiria kuacha muziki baada ya kutumbuiza katika Coachella mwaka wa 2019, miaka mitatu tu ya kazi yake ya muziki na hakujisikia kuridhika.
Mkali huyo wa muziki alisema aliamua kujikita katika teknolojia ili kupunguza uchovu aliokuwa akiupata kimuziki.
Alifichua haya katika mahojiano ya hivi majuzi na mwanahabari, Angela Lee.
Alisema, “Nina kampuni ya teknolojia inayoitwa Zagadat Capital. Na hii ilikuwa kama mimi kuchoka na muziki.
“Baada ya kutumbuiza katika Coachella mwaka wa 2019. Nilicheza siku ya kwanza ya Coachella, nilishuka kutoka jukwaani na sikuhisi chochote.
“Kwa hivyo, kwangu, ilikuwa ishara kwamba nitalazimika kuacha muziki na kwenda kufanya kitu kingine. Kwa sababu hiyo haikuwa hisia nzuri kuwa nayo au nilihitaji kusitisha. Labda nilikuwa nikipata uchovu.
“Na wakati COVID ilipoingia, ilikuwa mara ya kwanza nilisimama na kujaribu kuamua ni hatua gani inayofuata. Nilikuwa nimeanza Empawa kwa hiyo nilikuwa naelewa biashara ya muziki.
“Lakini nilichoka hata kusikiliza muziki. Unawezaje kuendesha biashara ya muziki bila kusikiliza muziki? Kwa hivyo, nilikuwa na timu yangu kushughulikia hilo.
“Siku zote nilitaka kuwa mjasiriamali na sasa muziki umenipa ufikiaji wa watu na mtaji, kwa hivyo nilikuwa kama, sawa, nitaanzisha mfuko wangu kama Jay-Z.”
Mr Eazi pia alifichua kuwa atawekeza kwenye tasnia ya filamu kuanzia mwaka ujao