Michezo

David Silva kaweka wazi wanachofikiria wachezaji wenzake kuhusu tetesi za Pep Guardiola kujiunga Man City …

on

Licha ya kuhusishwa kujiunga na kikosi cha Manchester United kocha wa FC Bayern Munich ya Ujerumani Pep Guardiola kwa asilimia kubwa anapewa nafasi ya kujiunga na kikosi cha Manchester City, kwani mambo yanatajwa kuwa katika mipango ya mwisho kukamilika.

Najua headlines za Pep Guardiola kujiunga na Man City umeshazisikia sana japokuwa hazijathibitishwa rasmi Guardiola atajiunga na klabu gani, licha ya kuwa tayari amethibitisha kuondoka katika klabu ya FC Bayern Munich mwisho wa msimu. December 21 tukiwa tunaelekea katika mchezo kati ya Man City dhidi ya Arsenal kiungo wa kimataifa wa Hispania anayekipiga katika klabu ya Man City David Silva amefunguka wanachofikiria wachezaji wenzake kuhusu tetesi za Guardiola.

Silva-Pellegrini-419051

“Kuhusu masuala ya kocha bado hayajawekwa wazi, tunaangalia kila siku kinachotokea mbele yetu na sio nini kitatokea siku za mbeleni. Tuna furaha na kocha Manuel lakini haina maana kwamba nimekuwa nikifikiria suala hilo, kwa sasa mechi dhidi yetu na Arsenal ndio kitu muhimu kwa sababu ndio mchezo wenye upinzani wa moja kwa moja” >>> Silva 

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments