Habari za Mastaa

VideoFUPI: Simu ya Rais Magufuli kwa Diamond kwenye clouds 360 ya Clouds TV

on

Leo March 14 2017 kupitia kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds TV, Rais Magufuli amepiga simu na kuzungumza na Mwimbaji wa Bongo fleva Diamond Platnumz baada ya kusikia Diamond akimuomba Rais Magufuli aisadie sanaa ya muziki kama anavyosaidia mambo mengine.

>>>”Mimi namuomba Rais Magufuli kama anavyosaidia mengine kwa wepesi, kwenye sanaa uweke mkono wako Baba tunakutegemea.” – Diamond.

Baada ya Diamond kuyaomba hayo, Rais Maguli alipiga simu moja kwa moja kwenye kipindi hicho na kusema:>>> “Nimemsikia Diamond na maombi yake nimeyapokea kwa mikono miwili nimefurahi kumskia siku ya leo natafuta siku ambayo tutakaa pamoja, nasikilizaga nyimbo zako hata wale wanaoigiza nawapenda sana na SHILAWADU.” – Rais Magufuli.

.>>>Hongera sana Diamond hongera sana kuwa na watoto, wakati wa kampeni ulikuwa na mtoto mmoja sasa una wawili.

Diamond pia amekiri kutokuwa na utofauti na Alikiba na kusema amemfahamu kupitia dada yake Queen Darleen na walishakutana Nairobi wakazungumza na anamkaribisha kuja kuuza muziki wake kwenye mtandao wa wasafi.com ……..

>>>’Sijawahi kuwa na matatizo na Alikiba ni chokochoko tu za watu, nina heshimiana naye na nimemfahamu kupitia dada yangu Queen Darleen, nilikutana naye Nairobi tukazungumza naye, Menejimenti yangu pia inajaribu kuongea na wao waje kuuza muziki wao kwetu’  

GoodNEWS: Nyingine kutoka WCB ya Diamond Platnumz, Bonyeza play hapa chini kutazama

VIDEO: Diamond alianza kwa kunilipa Elfu 5 na sikuona ni tatizo -KIFESI, Bonyeza play hapa chini kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments