AyoTV

Simba kuishitaki TFF kwa Nape, kama hili lisipotimia hawataendelea na mechi za Ligi (+Video)

on

Klabu ya wekundu wa msimbazi Simba March 16 kupitia kwa mkuu wao wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo Haji Manara wametangaza mambo mawili kuhusu TFF na Hassan Is-haka.

“kamati ya utendaji ya Simba imeamua kumpunguzia adhabu Hassan Is-haka na kumfungia mwezi mmoja, kumlipa nusu mshahara pamoja na kumvua unahodha, lakini baada ya kucheza mechi na Coastal Union hatutocheza mchezo wowote wa Ligi hadi Yanga na Azam FC ifikishe michezo sawa na sisi” >>> Manara

“tunaishitaki TFF kwa waziri Nape kwa kuipendelea Yanga na viongozi wake licha ya kufanya makosa. tumekuwa tukishitaki mambo kadhaa TFF lakini wamekuwa wakifumbia macho eti kwa sababu ni Yanga, tunajua Malinzi alikuwa katibu wa Yanga lakini hatutaki kuamini kuwa anapendelea” >>> Manara

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andikaAYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments