Michezo

Simba SC imeendeleza mabadiliko kwa kutangaza hatma ya Kitambi leo

on

Ikiwa ni siku chache zimepita toka uongozi wa Simba SC  utangaze rasmi kuachana na aliyekuwa kocha wao mkuu raia wa Ubelgiji Patrick Aussems kwa madai ya kuwa ameonesha vitendo vya utovu wa nidhamu na kushindwa kusimamia nidhamu katika timu.

Leo Simba SC imetangaza na kuonesha kuwa imeamua kufanya mabadiliko ya benchi zima la ufundi, Simba SC imethibitisha rasmi kuwa imeachana na kocha wake msaidizi Dennis Kitambi kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Simba SC imetangaza maamuzi hayo ikiwa zimepita saa chache kabla ya kumtangaza mchezaji wao wa zamani wa timu hiyo Seleman Matola kama ndio kocha wao mpya msaidizi.

VIDEO:YANGA SC YATANGAZA MADENI YAKE, CHIRWA, NGOMA, ROSTAND WANADAI

0

Soma na hizi

Tupia Comments