Michezo

Simba SC imemtangaza kocha mpya

on

Baada ya shauku ya muda mrefu na mashabiki wa soka wa Tanzania kutaka kujua ni nani atakuwa kocha mpya wa Simba SC baada ya kumfuta kazi akiyekuwa kocha wao Patrick Aussems hatimae jibu limepatikana leo.

Simba imemtangaza Sven Vanderbroeck ,40, raia wa Ubelgiji kama kocha wao
mkuu, Sven aliwahi kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Cameroon iliyotwaa Ubingwa waa AFCON 2017 nchini Gabon.

Sven pia amewahi kuwa kocha mkuu wa Zambia kuanzia 2018 hadi 2019, Simba haijaweka wazi imeingia mkataba wa muda gani na Sven, Sven amewahi kucheza soka katika vilabu kadhaa nchini kwake Ubelgiji ikiwemo Mechelen.

Soma na hizi

Tupia Comments