Michezo

Simba SC vs Coastal Union – hizi ndio takwimu za mchezo huo

on

IMG_8413COASTAL Union ya Tanga itakuwa na wakati mgumu wikiendi hii itakapokutana na Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Coastal haijawahi kupata ushindi wowote dhidi ya Simba tangu ipande daraja miaka mitatu iliyopita.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 1988 (wakati huo Ligi Daraja la Kwanza) walipanda daraja mwaka 2011 na tangu hapo imekuwa kwenye wakati mgumu inapokutana na Simba kwani haijashinda mchezo wowote kati ya mechi tano walizokutana ndani ya kipindi hicho cha miaka mitatu.

Katika michezo hiyo mitano iliyozikutanisha timu hizo tangu 2011 Simba imeshinda mara tatu huku michezo mingine miwili ikimalizika kwa sare. Simba iliifunga Coastal 1-0 Agosti 2011 kisha kuwafunga tena 2-1 Januari 2012.

Katika mchezo mwingine timu hizo zilitoka suluhu ya 0-0 Oktoba 2012 kabla ya Simba kushinda tena kwa mabao 3-1 Machi 2013.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzani Bara msimu huu, timu hizo zilitoka suluhu ya 0-0 mkoani Tanga.

Msemaji wa Coastal Union, Hafidh Kido alisema: “Timu iko vizuri kwa sasa na tumekuwa kwenye maandalizi mazuri hivyo tuna uhakika tutashinda mechi ya Jumapili.”

Kiungo wa Simba, Jonas Mkude amesisitiza kuwa kipindi cha mpito ilichokua inapitia timu yao kimekwisha na wachezaji wote wa timu hiyo wako kwenye morali ya juu hivyo wana uhakika wataibuka kidedea katika mchezo huo na michezo mingine iliyosalia msimu huu wala mashabiki wasikate tamaa.

SOURCE: MWANASPOTI

Tupia Comments