Michezo

Simba SC wababe wa Biashara 4-0

on

Simba SC leo imewakaribisha Biashara United ya Musoma katika uwanja wa Mkapa kukipiga katika muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu soka Tanzani bara 2020/21.

Biashara wakiwa ndio wageni wamekutana na kipigo cha magoli 4-0 kutoka kwa Simba SC ambaye ndio Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu.

Magoli ya Simba SC yalifungwa na Clatous Chama aliyefunga mawili dakika ya 9 na 26, Meddie Kagere dakika ya 52  na Mugalu aliyehitimisha kwa kupachika msumari wa mwisho dakika ya 85.

Soma na hizi

Tupia Comments