Klabu ya Simba SC na Kampuni ya
MobiAd Africa wameingia makubaliano ya udhamini kwa ajili ya kuendeleza soka la vijana katika Klabu hiyo.
Udhamini huo una thamani ya shilingi milioni 500 ukiwa ni mkataba wa muda wa miaka miwili.
“Soka la vijana ni muhimu sana. Ili uwe na timu ya vijana iliyo bora lazima iwezeshwe. Kama ilivyo kwa wachezaji wengine kama Mohamed Hussein kutoka kwa timu ya vijana.”- CEO Imani Kajula.
“Simba inakwenda mbele kutambua vipaji, kuvichukua na kuviendeleza na kuweza kutengeneza timu yenye vipaji vikubwa sana. Tunaamini Simba imara yenye vipaji haitaisaidia Simba pekee bali hata taifa letu.”- Imani Kajula.
“Leo tupo kwenye historia nyingine ya kuendeleza soka la vijana Tanzania. Mfumo wetu utakuwa mfumo wa wazi na endelevu.”- CEO Imani Kajula.