Michezo

Simba SC watokea mikwaju ya penati Shinyanga

on

Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo wamekutana na mtihani katika mchezo wao wa Kombe la FA dhidi ya Stand United katika uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga.

Simba Sc licha ya kucheza na Stand United iliyoshuka daraja wamelazimishwa sare ya kufungana goli 1-1 ndani ya dakika 90 lakini kwenye hatua ya mikwaju ya penati bahati ikaangukia kwa Simba waliopata ushindi wa 3-2.

Magoli ya ndani ya dakika 90 za mchezo yalifungwa na Hassan Dilunga dakika ya 52 kwa mkwaju wa penati kabla ya baadae dakika ya 67 Stand United kusawazisha kupitia kwa Miraji Salehe.

Soma na hizi

Tupia Comments