Michezo

Simba SC yamsamehe Morrison arejeshwa kikosini

on

Club ya Simba SC imetangaza kumrejesha kikosini mchezaji wake Bernard Morrison raia wa Ghana baada ya mchezaji huyo kuomba radhi.

Simba SC ilimsimamisha Morrison na kumpa siku 7 za kuandika barua na kueleza kwa nini asichukuliwe hatua zaidi za kinidhamu kwa tuhuma zinazomkabili za utovu wa nidhamu.

Taarifa ya Simba SC imeonesha kuwa mchezaji huyo ameomba radhi kwa CEO wa Simba SC Barbara Gonzalez, kocha Pablo Franco na benchi la ufundi kwa ujumla.

“Katika maelezo ya Morrison aliomba radhi kwa makosa yake na kuahidi kutorudia kwa maslahi mapana ya pande zote Mtendaji Mkuu amemsamehe Morrison na kumruhusu kuungana na wenzake”

Soma na hizi

Tupia Comments