Michezo

Simba SC yatangaza kurejea kwa mchezaji wake ‘Chama’

on

Club ya Simba imetangaza kurejea tena kikosini kwa Kiungo Mshambuliaji kutoka Zambia Clatous Chama akitokea RS Berkane ya Morocco alikokwenda huko miezi mitano iliyopita.

Chama alijiunga na Simba mwaka 2018 na kuondoka mwaka 2021 kabla ya kurejea Simba na kutambulishwa rasmi leo ambapo bango kubwa lililotolewa na Simba likiwa na picha ya Chama linasomeka “Karibu nyumbani, Welcome home”

Chama aliondoka Simba SC August 13 2021 na kujiunga na Club ya RS Berkane ya Morocco na sasa anarejea baada ya kudaiwa kushindwa kuzoea mazingira nchini Morocco.

 

AHMED ALLY: HUWA WANAKUJA WAMENG’ATA MENO, NILIWAAMBIA MAZOEZI YA PENATI WANAJISUMBUA KWA SIMBA HII

Soma na hizi

Tupia Comments