Michezo

Simba waifuata AS Vita nchini Congo DR, Mkude hayupo tayari anahitaji muda

on

Kikosi cha Simba SC kimeondoka leo nchini kuelekea Congo DR kuanza safari yake ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Ijumaa ya February 12.

Kuelekea mchezo huo Kocha wa Simba SC Didier Gomes aliongea na Waandishi wa Habari akiwa Airport jijini Dar es Salaam na kuulizwa vipi amemuonaje kiungo wake Jonas Mkude mara baada ya mazoezi ya siku kadhaa.

”Tunaenda Congo tukiwa na mipango kama sio kushinda basi kuondoka na walau kitu fulani, Mkude alicheza mchezo wa kirafiki jana dhidi ya U-20 (Simba B) alicheza kipindi kimoja na alikuwa vizuri lakini anahitaji muda zaidi sababu physical hayupo tayari”>>> Gomes

Simba SC wapo Kundi A katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2020/21 na Timu za Al Ahly ya Misri, AS Vita ya Congo DR na El Merreikh ya Sudan.

Soma na hizi

Tupia Comments