Club ya Simba SC imetangaza kumfuta kazi Kocha wake Mkuu Muhispani Pablo Franco Martin (41) ikiwa ni siku 207 toka ajiiliwe na Simba SC November 6 2021.
Pablo amefutwa kazi pamoja na Kocha wa viungo Daniel De Castro Reyes ikiwa ni siku mbili zimepita toka Simba SC ivuliwe Ubingwa wa Kombe la ASFC kwa kufungwa 1-0 na Yanga katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, huku Kombe pekee alilotwaa ni Mapinduzi Cup 2022 na kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Taarifa za ndani zinadai hajafutwa kazi tu kwa sababu ya kufungwa na Yanga ila Viongozi hawajavutiwa na mwenendo mzima wa timu yao ambao chini ya Pablo umepoteza matumaini ya kutetea taji lao la Ligi Kuu walilotwaa miaka minne mfululizo.