Klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wake, Barbara Gonzalez, imesema imeliandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuomba kufanyika kwa uchunguzi dhidi ya Wachezaji wa Al-Merrikh ya Sudan.
“Klabu ya Simba inapenda kuutarifu umma kuwa imepeleka barua rasmi Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kuomba uchunguzi kuhusu Klabu ya Al-Merrikh ya Sudan kuwachezesha wachezaji wawili waliofungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Sudan, katika mchezo namba 93 wa Klabu Bingwa ya Afrika dhidi yetu uliochezwa Machi 6, mwaka huu mjini Khartoum nchini humo,” Barbara kupitia taarifa hiyo.
Aidha taarifa hiyo ya Simba imewataja Wachezaji hao wanaodaiwa kucheza mchezo huo kinyume na utaratibu.
“Wachezaji hao ni Ramadan Ajab na Bakhiet Khamis ambao walifungiwa kutojihusisha na michezo kwa miezi sita kuanzia Januari 21, 2021 kutokana na kila mmoja kua na mikataba na timu mbili tofauti. Tunasubiri kupokea taarifa za uchunguzi kutoka CAF juu ya jambo hili na hatua stahiki zitakazochukuliwa,” Barbara