Top Stories

Simba Net wapata Mkurugenzi baada ya wa awali kuondolewa

on

Leo January 15, 2020 Nakusogezea taarifa Taarifa kutoka ndani ya Kampuni ya Wananchi Group Makao Makuu zinasema Mr.Kennedy Ojung’a ameteuliwa kuongoza Makampuni ya SimbaNET katika Nchi 5 za Africa ikiwa ni pamoja na Tanzania kama Mkurugenzi Mtendaji.

Kennedy atakuwa na majukumu ya kupanga mikakati ya kibiashara na kuifanya SimbaNET izidi kukua kwenye kanda na maeneo yote ambayo biashara inafanyika ikiwemo Tanzania.

Kennedy anachukua nafasi ya mtangulizi wake ambaye aliondolewa kwa tuhuma za ufisadi na udanganyifu.

AWESO ACHONGEWA NA WANANCHI KWA BASHIRU KISA KUZINGUANA NA MKANDARASI

Soma na hizi

Tupia Comments