Ad

Michezo

Ni kweli Emmanuel Okwi anarudi Simba? makamu wa Rais wa Simba ana majibu haya …

on

Wiki headlines za mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Uganda Emmanuel Okwi ambaye kwa sasa anacheza soka la kulipwa nchini Denmark, stori zake za kurudi Simba zinazidi zinazidi kuchukua headlines, Okwi ambaye aliuzwa na Simba katika klabu ya Sonderjyske ya Denmark aliripotiwa kuwa na mpango wa kurudi Simba na kuachana na klabu ya  Sonderjyske.

Stori za Okwi kutaka kurudi Simba ambayo amewahi kuitumikia kwa vipindi viwili tofauti, ziliandikwa sana katika magazeti, kitu ambacho kilikuwa kinaaminika na wengi kutokana na uongozi wa Simba kukaa kimya bila kutoa ufafanuzi, December 10 makamu wa Rais wa Simba Geofrey Kaburu amefunguka haya. Ni kweli wana mipango ya kumrejesha Okwi?

????????????????????????????????????

 

“Sisi kwa maana ya uongozi wa klabu ya Simba kwa suala la usajili tumeshakamilisha na majina yamepelekwa TFF, ukweli wa Okwi ni kwamba hakuna mazungumzo rasmi ya uongozi juu ya kurudi kwa Emmanuel Okwi, hayo ni maneno mnayosikia pembeni hayo ni romours, kuhusu kufanya mawasiliano yapo ya kawaida yaani ya kirafiki kwa sababu haikatazwi ila kurudi Simba kwa mkataba mpya hilo halipo mezani kwa upande wetu” >>> Kaburu

Emmanuel Okwi aliuzwa na Simba kwa mara ya kwanza mwaka 2o13 kwenda katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa dola 300000 ila baadae alivunja mkataba wake na klabu hiyo na kurudi kwao Uganda baada ya kushindwa kumlipa mshahara wake, baadae akaja Yanga na kurudi Simba na July 10 2015 Simba ilimuuza kwenda klabu ya Sonderjyske ya Denmark.

IMG_57731

Okwi akikabidhiwa jezi ya Sonderjyske ya Denmark.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments