Michezo

Mambo matatu ya kufahamu kutoka Simba, kuhusu Mavugo, Hassan Kessy na Kiongera (+Audio)

on

Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba imekuwa ikihusishwa kwa mambo kadhaa sasa kuhusiana na dirisha dogo la usajili, wengi wamekuwa wakiitaja Simba kuwa kwa sasa haina mshambuliaji mkali zaidi ya Hamisi Kiiza hivyo huenda ikamsajili mrundi Laudit Mavugo katika dirisha hili kutokana na tetesi kuwa mkataba wake una malizika na klabu ya Vital’O.

Stori zimekuwa nyingi ikiwemo taarifa ya kumrejesha mshambuliaji wake Paul Kiongera raia wa Kenya waliyekuwa wamemtoa kwa mkopo Kenya ila sasa anarejea, millardayo.com ilimtafuta Mkuu wa Idara ya Habari wa Simba Haji Manara azungumzie mambo matatu, kuhusu kumsajili Laudit Mavugo, mkataba wa Hassan Kessy na nani atarithi mikoba ya Selemani Matola katika nafasi ya ukocha msaidizi atatoka nje ya nchi au?

“Kessy bado ana mkataba wa miezi saba na Simba hivyo hakuna klabu inayoruhusiwa kuongea nae sababu bado mchezaji wa Simba na akirejea kutoka Algeria tutamuongezea mkataba” >>> Manara

DSC_0044

“Kiongera ndio anarudi kuhusu mshambuliaji mpya ndio tuna mpango huo ila subirini tutawaambia kama ni Mavugo mtajua tu ila ndani ya siku mbili hizi Kiongera ataanza mazoezi na wenzake” >>> Manara

“Kweli tumtafuta kocha msaidizi ila ni ndani ya nchi kuhusu nani kapendekeza ni kamati ya utendaji mwalimu yeye anatoa maoni ambayo yanabakia ndani ya klabu ila Simba ndio ina maamuzi ya kumchagua kocha msaidizi hivyo wakati wowote kutokea sasa tutawaambia” >>> Manara

Sauti ya Haji Manara

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments