Michezo

Pichaz za Simba walivyojiandaa kuikabili Yanga Jumamosi hii

on

Jumamosi ya September 26 ni siku ambayo unachezwa mchezo wa kihistoria katika soka la Tanzania, ikiwa ni siku ambayo baadhi ya vilabu vya Ligi Kuu vitashuka uwanjani kucheza mchezo wa round  ya nne, katika uwanja wa taifa Dar Es Salaam utapigwa mchezo ulioteka hisia za kila mpenda soka Tanzania kwani ndio siku mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga itapigwa uwanja wa Taifa.

6

Huu ni mchezo wa kihistoria kwa vilabu vya Simba na Yanga kwani vimewahi kucheza mara 79, Simba ambaye ndio atakuwa timu mwenyeji wa mchezo huo amewahi kumfunga Yanga mara 23, Yanga imewahi kumfunga Simba mara 29 na sare zimetoka mara 27. Hadi sasa vilabu hivyo vimecheza mechi 3 katika Ligi Kuu soka Tanzania Bara kwa msimu wa 2015/2016.

5

Simba na Yanga zote zimeshinda mechi zao tatu za mwanzo, hivyo Yanga wamekimbilia Pemba kwenda kuweka kambi na wekundu wa Msimbazi Simba, wameweka kambi Unguja, ninazo picha sita za wekundu wa Msimbazi Simba wakijifua katika uwanja wa Amani Zanzibar September 24.

3

4

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata,pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE

Tupia Comments