Michezo

Shabiki wa Timu ya Simba ikufikie hii, na wewe unashiriki kumpata mchezaji Bora wa Mwezi..

on

Ikiwa ni katika muendelezo na harakati za kuipeleka klabu ya soka ya Simba katika mfumo wa kisasa na kujenga kikosi chenye wachezaji wenye morali uwanjani, mwezi September klabu ya Simba imetangaza kuanzisha mfumo wa kumtafuta mchezaji bora wa mwezi.

Kupitia kwa Rais wa klabu hiyo Evans Aveva ametangaza kuanzisha mpango huo mwezi September, ambapo mfumo utakaotumika kumpata mchezaji bora wa mwezi ni mashabiki ndio watakuwa na nafasi ya kumchagua kwa kumpigia kura kwa njia ya sms.

“wanachama na wapenzi wa Simba wanathamini mno mchango wa wachezaji katika kuifanya timu yetu ifanye vizuri, hivyo tumeona ni jambo la busara kuwa klabu ya kwanza Nchini Tanzania kuwa na tuzo ya mchezaji bora wa mwezi. Tunaamini kuwa Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Simba itaongeza morali na kujituma kwa wachezaji wetu” >>> Evans Aveva

DAKA RATIBA -02_2

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE

Tupia Comments