Michezo

Matokeo ya Simba na Jkt Oljoro yapo hapa.

By

on

simba2Ile mechi iliyo kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyokuwa inachezwa kati ya timu ya Simba na Jkt Oljoro kutoka 87.9 Arusha imekamilika leo kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Matokeo ya leo Simba wamefanikiwa kuifunga Jkt Oljoro magoli 4-0 ambapo hadi timu zinaenda mapumziko tayari Simba walikuwa wakiongoza kwa magoli 3-0,huku magoli matatu ya leo yakifungwa na Amisi Tambwe na moja alifunga Jonas Mkude.

Kwa matokeo haya yanaifanya Simba iwe na jumla ya pointi 30 baada ya kucheza mechi 15 ikiwa nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City pointi 31, Yanga SC pointi 32 pamoja na Azam FC pointi 33 ambao wanaongoza ligi kwa sasa.

Upande wa Tambwe leo alifunga bao lake la kwanza leo na la pili kwa timu yake ya Simba dakika ya 22 na goli la tatu alifunga dakika ya 28,Kipindi cha pili Simba SC walirudi na kufanikiwa kupata bao la nne dakika ya 52 mfungaji akiwa Tambwe tena.

 

Tupia Comments