Michezo

Baada ya headlines za bilionea wa 24 Afrika kutaka kuinunua klabu ya Simba, hii ndio kauli rasmi ya Simba …

on

Baada ya stori nyingi kuingia katika headlines kwa siku za hivi karibuni kuhusu uamuzi wa moja kati ya mabilionea wa Afrika kutaka kuinunua klabu ya Simba, mengi yameandikwa na mengi yameongewa, najua unahitaji kufahamu kuhusu stori za bilionea Mohamed Dewji ambaye maarufu kama MO kuweka bayana dhamira yake ya kutaka kuinunua Simba kupitia kipindi cha Mkasi TV.

Kama unatamani kujua majibu ya viongozi wa Simba kuhusu stori za MO kutaka kuinunua Simba, ukweli kutoka kwa msemaji wa Simba Haji Manara anasema bado klabu haijapokea barua rasmi kutoka kwa MO wala huyo bilionea mwingine anayetajwa kutaka kuinunua Simba.

DSC_0168

Haji Manara

“Ukweli ni kuwa hakuna mfanyabiashara yoyote au tajiri yeyote aliyetuma barua rasmi ya kuomba kuinunua Simba, haya maneno yanazungumzwa tu, kama klabu hatujapata barua. Ni kweli binafsi nimeiona interview ya MO ila interview ya MO haitoshi kusema ndio taarifa yake rasmi, ukweli bado klabu haijapokea barua yoyote ya mtu kuomba kuinunua Simba” >>> Haji Manara

rellr_Mohammed-Dewji_office-1000x600

Mohamed Dewji ‘MO’

Kwa taarifa zisizo rasmi ni kuwa Simba inawaniwa na mabilonea wawili MO ambaye amewahi kukiri wazi kupitia kipindi cha Mkasi TV, ila bilione mwingine jina lake halijawekwa wazi. Kama utakuwa unakumbuka vizuri Mohamed Dewji ‘MO’ mwezi March 2015, alitajwa na jarida la Forbes la Marekani kuwa moja kati ya mabilionea 29 wa Afrika akiwa nafasi ya 24 kwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 1.3 ambazo ni sawa na Tsh trilioni 2.34.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments