Michezo

Simba yaendeleza usajili kimya kimya kwa kumsajili mshambuliaji huyu kutoka Kongo

on

Tukiwa tunaelekea kuanza kwa Ligi Kuu soka Tanzania bara vilabu kadhaa vimezidi kujizatiti kwa kusajili wachezaji wenye viwango vya juu. Klabu ya soka ya Simba ambayo bado ipo katika hali ya sintofahamu juu ya mshambuliaji Laudit Mavugo raia wa Burundi lini atatua Dar Es Salaam, Simba imetangaza kumsajili mshambuliaji mwingine.

IMG-20150625-WA0062

Simba imemsajili mshambuliaji Danny Lyanga kutoka katika klabu ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Lyanga amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Simba na atasafiri August 2 kuelekea visiwani Zanzibar kuungana na wachezaji wenzake walioweka kambi visiwani humo.

Zikiwa zimebaki siku nne kufungwa kwa dirisha la usajili, klabu ya Simba ndani ya siku tatu imesajili wachezaji watatu ambao ni kiungo kutoka Zimbabwe Justice Majabv na beki kutoka Burundi Emery Nimubona.

IMG_1903

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

 

Tupia Comments