Michezo

Chanzo cha ajali mashabiki wa Simba, vifo na majeruhi vimetajwa.. #RIP

on

AJALI DOMHii ilianza kuchukua Headlines jana April 03 kuhusu ishu ya ajali ambayo walipata mashabiki wa Timu ya Simba waliokuwa wakisafiri kwenda Shinyanga kushabikia Timu yao ambayo itakuwa ikipambana na Kagera Sugar leo April 4.

Leo imetawala pia katika vyombo vya Habari, Ripota wa Clouds FM Morogoro aliripoti tukio hilo, amesema ajali hiyo imetokea mbele kidogo ya Morogoro ambapo mvua inaendelea kunyesha, utelezi wa Barabarani ukafanya gari hiyo kupata ajali.

Watu saba wamefariki na wengine 18 ni majeruhi ambao walipelekwa Hospitali kwa ajili ya matibabu.

Kama hukuisikia taarifa hii play hapa..

Pole kwa watu wetu waliopata ajali hii.. #RIP

Kaa karibu na millardayo.com, nitakachokipata nitakusogezea hapa muda wowote kuanzia sasa, unaweza kujiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments