Michezo

Simba yamrejesha mkongwe mwingine kikosini

on

11150620_949579691743163_5341729428873410419_n

Klabu ya soka ya Simba imezidi kuimarisha kikosi chake kwa kuwasajili nyota kadhaa msimu huu… Simba ambayo ipo visiwani Zanzibar kwa maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara inajipanga kurejesha heshima ya kikosi chake ambayo siku za karibu kimekuwa hakifanyi vizuri.

Mwinyi-2ee36

Baada ya kumsajili nahodha wake wa zamani Musa Hassan Mgosi sasa imemrejesha mkongwe mwingine Mwinyi Kazimoto aliyeondoka miaka miwili iliyopita na kutimkia  Al Markhiya ya QatarMwinyi amejiunga na Simba kama mchezaji huru na amesaini mkataba wa miaka miwili.

MwinyiKazimoto

Ikumbukwe kuwa Mwinyi amewahi kuichezea Simba akitokea JKT Ruvu mwaka 2011-2012 kabla ya mwaka 2013 kutimkia  Al Markhiya ya Qatar.

Mwinyi-Kazimoto

 

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments