Michezo

Uamuzi huu ulitolewa na Simba baada ya mashabiki wao kupata ajali..

on

Mashabiki watano na watu wengine wawili walifariki katika ajali ya gari iliyotokea jana katika eneo la Dakawa Morogoro, leo ilikuwa ichezwe mechi kati ya timu ya Simba na Kagera Sugar katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Taarifa kutoka Bodi ya Ligi Tanzania zimeeleza mechi hiyo iliyokuwa ipigwe leo kwenye Uwanja wa Kambarage imeahirishwa kutokana na ajali ya mashabiki wa ‘Simba Ukawa‘.

Ajali hiyo ilitokea wakati mashabiki hao wakiwa wanaenda kuiona mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara.

Katika hatua nyingine Ligi kuu ya Vodacom imeendelea leo hii kwa Ndanda FC ambao waliikaribisha Mbeya City Mtwara na kutoka sare ya  1 – 1, Mbeya City, Coastal Union wamefungwa nyumbani 0 – 1 na Prisons, huku Ruvu Shooting  wakiitandika 1 – 0 JKT Ruvu.

Kaa karibu na millardayo.com nitakachokipata nitakusogezea hapa muda wowote kuanzia sasa, unaweza kujiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments