Michezo

Simba bado hali tete, haya hapa matokeo yao dhidi ya Stand United na mechi zingine za VPL

on

Screen Shot 2014-10-04 at 7.27.30 PMHali imezidi kuwa mbaya kwa klabu ya Simba, ikiwa haijashinda mchezo katika msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom, wana msimbazi leo walijitupa kwenye uwanja wao wa nyumbani wakiwakaribisha wageni kwenye ligi kuu Stand United.

Huku ikiwa na rekodi ya kushindwa kulinda ushindi wake katika mechi mbili zilizopita – wakianza kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Coastal Union, kisha sare ya 1-1 dhidi ya Polisi Morogoro, Simba leo tena walianza kuongoza kwa goli moja lilofungwa na Shabaan Kisiga katika dakika ya 35.

Lakini ilivyo kawaida yao msimu huu, dakika 10 baadae beki yao ikazembea na Stand United wakapata goli la kusawazisha kupitia mchezaji na Omary Mtaki.

Matokeo mengine kwenye ligi hiyo ni kama ifuatavyo:

Polisi Morogoro 1-1 Kagera Sugar… FT… Coastal Union 2-1 Ndanda FC… FT… Ruvu Shooting 0-0 Mbeya City

Tupia Comments