Ni Septemba 27, 2023 ambapo Afisa Habari wa Simba Sport Club, Ahmed Ally amezungumza na vyombo vya habari, hizi ni nukuu zake katika mkutano huo.
“Mchezo dhidi ya Power Dynamos utachezwa siku ya Jumapili Oktoba mosi saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex. Tumeamua kucheza saa 10 sababu michezo mingi hapa karibuni tumecheza muda huo hivyo hatukutaka kubadili muda lakini pia Jumatatu itakuwa siku ya kazi hivyo tunataka watu wawahi kurudi nyumbani.”- Ahmed Ally.
“Kuelekea kwenye mchezo huo ambao ndio utafatiliwa zaidi Afrika kwa wikiendi hii kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza. Ukubwa wa Simba SC ndio unafanya mchezo huo uwe mkubwa zaidi.”– Ahmed Ally.
“Kikosi leo kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Azam Complex pale Chamazi kwa ajili ya kuzoea uwanja. Tangu tumeanza msimu huu hatujawahi kutumia ule uwanja. Wapo wachezaji wetu wengi wanaujua uwanja ule na wpao wengine hawaujui.” – Ahmed Ally.
“Wachezaji watatu watakosekana kwenye huo mchezo. Wachezaji hao ni Aishi Manula, Henock Inonga na Aubin Kramo.”- Ahmed Ally.
“Tarehe moja ya mwezi wa kumi ni siku ya Mnyama kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Sisi hatwendi kuweka historia, tunakwenda kwenye miasha yetu ya kawaida.”- Ahmed Ally.
“Tunafahamu mchezo ni mgumu dhidi ya Power Dynamos, wote mliona namna walivyotusumbua lakini wanakuja nyumbani Tanzania, sehemu ambayo hakuna aliyetoka salama na hicho hicho atakutana nacho. Bora wangekubali tukamalizana nao kwao.”- Ahmed Ally.
“Ule Uwanja ni wa Azam FC, Simba SC tutakwenda kucheza pale kutaka matokeo tu, amecheza nani, ameutumia nani hilo halitupi wasiwasi. Ule uwanja sio wa nyuma mwiko, sisi tutacheza na tutaingia hatua ya makundi. Wala mashabiki wasiwe na mashaka hata kidogo.”- Ahmed Ally.
Hatutafanya hamasa kubwa maana tunaweza kuwatia watu mzuka alafu tutakosa sehemu ya kuwaweka, itakuwa ya kawaida sababu watu 7,000 tutajaza kwa haraka.”
“Mechi hii tutaitumia kama maandalizi ya kwenda kucheza CAF Football League.”- Ahmed Ally.