Michezo

Matokeo ya mechi ya Simba Vs Yanga yapo hapa pamoja na mechi nyingine za Ligi Kuu Sept 26 (+Pichaz)

on

Jumamosi ya September 26 ni siku ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wa soka Tanzania, kwani ndio siku ambayo tumepata nafasi ya kuona mechi ya kihistoria ya watani wa jadi Simba dhidi ya Yanga mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.

IMG_1936

Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli la Amissi Tambwe upande wa mashabiki wa Simba

Kabla ya kuchezwa kwa mechi hiyo ya kihistoria ambapo klabu ya Simba ndio ilikuwa timu mwenyeji wa mchezo huo, Simba na Yanga wamewahi kukutana mara 79, lakini klabu ya Dar Es Salaam Young Africans kwa mujibu wa rekodi inaonekana kuwa mbabe kwa kuifunga Simba mara 29, huku Simba wakiwa wamewahi kuifunga Yanga mara 23 na kutoka sare mara 27. Hii ndio rekodi ambayo Simba na Yanga ziliingia uwanjani zikiwa zinaijua.

w

Golikipa wa Yanga Ali Mustapha akitoa mpira katika eneo la hatari

Mchezo umemalizika kwa klabu ya Dar Es Salaam Young Africans kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 2-0 dhidi ya watani wao wa jadi Simba, magoli ya Yanga yalifungwa na Amissi Tambwe dakika ya 44 kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Malimi Busungu na kuandika goli la kwanza.

434

Mbuyu Twite akitolewa nje na daktari wa Yanga Juma Suphian baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu.

Goli la pili lilifungwa na Malimi Busungu kwa kichwa baada golikipa wa Simba Peter Manyika kushindwa kuucheza mpira huo na kuingia wavuni dakika ya 79. Mechi ilimalizika kwa Mbuyu Twite kupewa kadi nyekundu baada ya kuchelewesha muda ukizingatia alikuwa na kadi ya manjano.

DSC_0087

mashabiki wa Yanga baada ya ushindi wa goli la Busungu

 Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizochezwa September 26

  • Coastal Union 0 – 0 Mwadui FC
  • Tanzania Prisons 1 – 0 Mgambo Shooting
  • JKT Ruvu 0 – 1 Stand United
  • Mtibwa Sugar 1 – 0 Maji Maji FC 
  • Kagera Sugar 0 – 0 Toto Africans

Hizi ni pichaz za mechi ya Simba Vs Yanga

DSC_0146

Shabiki wa Simba aliyerusha chupa ya maji uwanjani akiwa kakamatwa na askari polisi

DSC_0105

Hamis Kiiza akimuangalia golikipa wa Yanga aliyechini baada ya kupata maumivu

DSC_0095

Mussa Hassan Mgosi akifanya mipango ya kumpita Mbuyu Twite

DSC_0111

Wachezaji wa Simba na Yanga wakimzonga refa baada ya kufanyiwa faulo mchezaji wa Yanga

DSC_0088

Mashabiki wa Yanga

DSC_0077

Nadir Haroub akimdhibiti Hassan Kessy

DSC_0021

Hamis Kiiza akimkumbatia kocha wake wa zamani Hans van der Pluijm

DSC_0033

Sserunkuma na Jonas Mkude wakiwa benchi

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata,pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE

Tupia Comments