Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imeshindwa kusikikiza kesi ya kusambaza taarifa za uongo inayomkabili aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt.Wilbroad Slaa (76) kwa sababu ya kutofikishwa mahakamani.
Dkt.Slaa alifikishwa mahakamani hapo Januari 10, 2025 akikabiliwa na kesi ya jinai namba 993 ya mwaka 2025, ambapo alitarajiwa kufikishwa mahakamani hapo leo kwa ajili ya kujua hatma ya dhamana yake baada ya Upande wa Jamhuri kuwasilisha kiapo cha kuzuia dhamana.
Katika kesi hiyo, Dkt.Slaa anatetewa na Jopo la Mawakili sita, linaloongozwa na Biniface Mwabukusi, Peter Madeleka, Hekima Mwasipu, huku Jamhuri ikiwakilishwa na Wakili Tawabu Issa.
Wakili wa Serikali, Issa alisema kuwa kesi hiyo imeitishwa leo kwa ajili ya mjadala wa dhamana lakini mtuhumiwa hajafika mahakamani licha kwamba wameuliza lakini wameambiwa hajafika.