Ad

Michezo

Baada ya Sir Alex Ferguson kusikia wanataka kumtimua Mourinho, kaongea haya maneno 77 tu.

on

Kwenye headlines za Sports leo na hii kauli ya kocha wa zamani wa Manchester United imo kwenye zile stori kubwakubwa… ni baada ya stori zinazoendelea kusambaa kuhusu Chelsea kuwa na mpango wa kumtimua kocha Jose Mourinho baada ya timu hiyo kutokufanya vizuri.

ferguson 2

Baada ya hizo fununu za Mourinho kutimuliwa kumfikia na kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson, amesema yafuatayo >>> ‘Tajiri wa Chelsea amefukuza makocha wengi sana ndani ya miaka kumi iliyopita na nina uhakika amejifunza kwa kipindi hicho’

mourinho

Ferguson anaendelea kwa kusema ‘Anatakiwa kujua hiki ni kipindi cha mpito tu kinapita na awe na imani na Mourinho kwamba atakaa sawa tu, hainishawishi kumfukuza kazi mmoja wa makocha bora wa wakati wote.. ameshinda makombe ya Ulaya mara mbili, ameshinda ligi kwenye kila nchi alikofundisha timu, itakua ni ujinga kumfukuza Mourinho kazi, itaonyesha kabisa wewe ni bosi mbovu usiejua nini cha kufanya’

UNAONAJE ALIYOYASEMA FERGUSON? NIACHIE COMMENT YAKO MTU WANGU

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments