Nchi nyingi Duniani utaratibu wa saa za kazi kwa siku ni saa nane tu, asubuhi mpaka jioni… lakini zipo Kampuni au Mashirika binafsi ambayo yametengeneza utaratibu wake wa saa za kazi, lakini kwa Serikalini mara nyingi utaratibu ni mmoja.
Sikuwa najua kumbe Ofisi ya Kampuni ya Toyota iliyopo Jiji la Gothenburg Sweden walibadili utaratibu wa kazi kwa Wafanyakazi wao miaka 13 iliyopita, Wafanyakazi wao wanafanya kazi kwa saa sita tu kwa siku na wameona mafanikio makubwa ikiwemo Wafanyakazi kuwa na moyo zaidi wa kufanya kazi!!
Jiji la Gothenburg ndani ya Sweden huenda wakabadili mfumo pia na sehemu nyingine za kazi kutokana na majibu yatakayopatikana kwenye utafiti ambao umeanza kufanywa kuanzia mwaka 2014 mpaka 2016 ambapo Manesi wamepunguziwa saa za kazi kutoka saa nane kwa siku mpaka saa sita.
Kingine ambacho kimependekezwa ni kwamba ili utendaji kazi uwe mzuri kwa hizo saa sita kwa siku, Wafanyakazi wanatakiwa wapunguze kuwa busy na mambo binafsi wakiwa Ofisini ndani ya saa za kazi, ikiwemo kuchat kwenye Mitandao ya Kijamii kama vile Facebook.
Japo kuna Makampuni mengi ndani ya Sweden yameanzisha huu utaratibu wa kufanya kazi saa sita kwa siku ambazo kwa wiki ni jumla ya saa 30, bado Makampuni mengi makubwa utaratibu wao ni wa saa nane kwa siku ambazo kwa wiki ni saa 40.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE