Habari za Mastaa

Skales azungumzia mtazamo wake juu ya wimbo Shake Body!

on

Skales

Skales ni mtunzi wa nyimbo na rapper kutoka Nigeria aliyeanza kuandika nyimbo miaka ya 2000 mpaka 2007, mwaka 2014 alihamia kwenye lebo ya Baseline Music na chini yao alihit na ngoma yake ya Shake Body iliyoweka headlines kubwa Africa.

Kwenye interview moja aliofanya Nigeria, Skales aliongelea sababu zilizomfanya aachie ngoma ya Shake Body, wimbo ambao yeye binafsi hakutokea kuupenda kabisa. Skales alisema haya;

>>> ” Wimbo wa Shake Body kwangu ulikuwa wimbo mbaya sana kwa sababu sikuipenda kazi niliyoifanya kwenye wimbo ule, nikaja kukutana na Dj Kentucky ambaye aliomba kuusikiliza wimbo huo,akaupenda na akaniambia niutoe, nikapotezea, badaae nikakutana na Timaya naye akausikiliza akasema ni hit na kuniomba nisimalize mwezi sijauachia, tena nikapotezea! Lakini baada ya kupata mitazamo ya watu wengi waliodhani wimbo utafanya vizuri nikaamua kuitoa, na nilishangazwa jinsi watu walivyoipokea vizuri ngoma hio!” <<< Skales.

Nimekusogezea video hiyo hapa chini mtu yangu.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

 

Tupia Comments