Videos

VideoMPYA: Sio tena Bongofleva, ni Gospel kuanzia leo – Seline

on

May 2016 jina la Seline lilikua miongoni mwa majina matatu ya Wasanii wapya waliotambulishwa chini ya Label ya THE INDUSTRY ambapo wengine walikua ni Rosa Ree na Wildad lakini mwishoni mwa hiyohiyo 2016 Seline aliondoka kwenye Label hiyo.

Baadae Seline aliendelea na harakati za Bongofleva lakini habari mpya ya sasa ni kwamba ameachana na Bongofleva na ameanza rasmi kuimba nyimbo za Injili.

Nimeamua kumtumikia Mungu sababu kanifanyia mengi sana katika maisha yangu na maisha yangu ni ushuhuda….. sasa kwa sababu mimi ni msanii basi nimeamua kutumia kipaji changu kutangaza utukufu wake na nimetoa wimbo unaitwa JITUME simply means FAITH WITH OUT WORK IS DEAD asiyefanya kazi na asile

Mungu ndio anaejua hata kama maisha magumu kiasi gani muamini yeye daima usisikilize ya binadamu sababu mwanadamu hana uwezo wakukupadisha wala kukushusha, never give up hata ukipitia majaribu amka, sali na kazana”  – Seline

Itazame hapa chini video mpya ya Seline baada ya kutangaza kuanza kuimba nyimbo za Gospel na ukishamaliza kuitazama usiache kutupia comment yako ukisema ulivyoipokea.

VIDEO: Q Boy kuhusu Dancer wa Justin Bieber kuucheza wimbo wake

Soma na hizi

Tupia Comments