Michezo

Hivi huyu Bondia nd’o kusema alisahau akapanda na smartphone ulingoni au? Cheki hii video

on

BOXEO MEDIANO COLOMBIA - PARAGUAY

Labda tuulizane hapa mtu wangu, hivi zile bukta wanazovaaga mabondia wakiwa ulingoni zina mifuko kweli ya kuwekea vitu?

Hili swali nimejiuliza baada ya kukutana na hii video ikionesha bondia mmoja akiangusha simu wakati pambano lao likiendelea.

Pambano lilikuwa kati ya Ramon Luis Nicolas na  Marvin Jones ambapo Marvin aliangusha smartphone yake raundi ya kwanza kabisa ya mchezo, referee akaiokota na kumpa jamaa.

Swali ni kwamba yani mpaka anaingia uwanjani simu hakuiona kweli?

Cheki hii video hapa…

Kaa karibu na millardayo.com nitakachokipata nitakusogezea hapa muda wowote kuanzia sasa, unaweza kujiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments