Top Stories

Simba SC yatangaza kumpiga chini Mzee Kilomoni

on

Miezi kadhaa baada ya kuvutana sana na uongozi wa klabu ya Simba uliopo madarakani sasa kuhusu mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo, hatimaye leo July 16, 2019 klabu ya Simba kupitia CEO wao Crescentius Magori wametangaza rasmi kumuondoa kwenye sehemu ya baraza la wadhamini la klabu.

“Hapa karibu tumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusu Hamis Kilomoni kuwa mdhamini wa klabu yetu ya Simba, Hamisi Kilomoni ambaye alikuwa ni mdhamini wa Baraza la Simba, amekuwa akipita kwenye vyombo vya habari akieleza habari za klabu yetu” Magori 

“Kuanzia leo tunatangaza kuwa Mzee Kilomoni sio tena mdhamini wa Baraza la Simba na mkataba wake haupo tena, maana mkataba ulikamilika October 2017” 

“Na kwa msisitizo zaidi maswala yake tumeyafunga leo hatutaliongelea tena suala zaidi hatua za kisheria zitafuata.” Magori

“NIMEZUNGUMZA HADI KOO LIMENIKAUKA”-WAZIRI BASHUNGWA

Soma na hizi

Tupia Comments