Ukishakuwa chini ya ulinzi kituo cha Polisi kuna vitu ambavyo hauko huru kufanya kwa sababu tu ya sheria za maeneo hayo.. hii stori iko kwenye headlines za vyombo vya Kenya, mitandao imeandika pia.
Inamhusu Henry Magee, alikuwa anashikiliwa na Polisi kwa kesi ya kumteka mwanafunzi wa kike.
Kesi ambayo iliongezeka kwa huyu bwana ilikuwa ni ishu ya kuvuta sigara akiwa selo.. akafikishwa tena Mahakamani na kutozwa faini ya Sh 15,000 za Kenya katika Mahakama ya Eldoret baada ya kukubali kufanya kosa hilo.
Mtuhumiwa huyo Henry Magee alitozwa faini hiyo na Hakimu Tom Olando, ambae amesema alisikia harufu ya moshi wa sigara akiwa kwenye chumba chake cha kusikilizia kesi, chumba hicho kiko jirani na selo ambayo Henry alikuwa amefungiwa.
Jamaa alipewa nafasi ya kujitetea; “Ni kweli nilifanya makosa ambayo yametajwa dhidi yangu lakini ni kwa sababu ya mazoea ya kutumia sigara,”– Magee.
Kitu ambacho nimejiuliza ni kwamba watu wengi akishakua yuko selo anakuwa na uoga hivi, sasa huyu jamaa kapataje ujasiri wa kuvuta sigara kabisa ndani ya chumba cha jela !!
millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook