Michezo

AMERUDI: Ajibu amesaini Simba SC miaka miwili

on

Ibrahim Ajibu Migomba amerejea Simba SC na amesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia wekundu hao wa msimbazi. Ajibu alijiunga na Yanga SC Julai 2017 akitokea Simba ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili.

“Safari ya mtoto kuishi mbali na nyumbani imefikia ukingoni, Ibrahim Ajibu ameamua kufanya maamuzi sahihi ya kurudi nyumbani Msimbazi, ndio amerudi na amesaini mkataba wa miaka miwili kucheza na kuwapa furaha Wanasimba, karibu nyumbani Ajibu” ni maneno yaliyoandikwa katika  ukurasa rasmi wa klabu ya Simba SC ikiambatanishwa na picha za Ajibu akisaini mkataba

TAIFA STARS YATOLEWA KINYONGE AFCON, HII NDIO KAULI YA SAMATTA

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments