Michezo

Mavugo, Blagnon na Kichuya wameipatia Simba point 3 uzinduzi wa VPL

on

Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017 leo August 20 ndio ulianza rasmi kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali Tanzania.    

Uwanja wa Taifa Dar es Salaam wekundu wa Msimbazi Simba SC waliwakaribisha Ndanda FC wanakuchele kufungua pazia la Ligi Kuu msimu wa 2016/2017.    

Katika mchezo huo ambao Simba SC waliwatumia wachezaji wao maprofeshino katika nafasi za ushambuliaji walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-1, magoli ya Simba yalifungwa na Laudit Mavugo dakika ya 19 , Fredrick Blagnon dakika ya 73 na Shiza Kichuya dakika ya 79 wakati goli pekee la Ndanda FC lilifungwa na Omary  Mponda dakika ya 36.

WhatsApp Image 2016-08-20 at 18.52.06

ULIIKOSA HII APPLICATION ILIYOZINDULIWA KWA AJILI YA KUZUIA AJALI BARABARANI

Soma na hizi

Tupia Comments