Habari za Mastaa

PICHA: Baada ya mauaji, Snoop Dogg na The Game waongoza watu mpaka Polisi

on

Baada ya mauaji ya Wamarekani weusi wawili juzi ambayo yamepelekea kuuwawa kwa Polisi watano kwenye mji wa Dallas Marekani kama njia ya kulipa kisasi, Wanahiphop maarufu kutoka jimbo la California Marekani The Game na Snoop Dogg wameongoza kundi la Wanaume kwenye matembezi ya amani mpaka makao makuu ya Polisi.

Snoop 6

Moja ya post za The Game akisema ‘sisi sio Wanyama’

Rapper The Game aliitisha matembezi hayo kupitia Instagram yake na kusema wanaotakiwa kushiriki kwenye matembezi hayo ni Wanaume tu, Wanawake na watoto wabaki nyumbani na kwamba Mwanaume yeyote atakaekuja hatakiwi kuwa na silaha yoyote.

Snoop 7

snoop 2

The Game na Snoop Dogg wakiongoza matembezi ya amani kuelekea makao makuu ya Polisi Los Angeles California.

Ni matembezi yaliyokua na kusudi la kuondoa hofu baada ya mauaji kutokea na kuurudisha umoja na ushirikiano kati ya Polisi na Wananchi, kuanzisha uhusiano mpya na kuondoa hofu ya kuwindana baina ya Polisi na raia.

Snoop 1

Kwenye hii movement yao iitwayo H.U.N.T (Hate Us Not Today) viongozi Snoop Dogg na The Game walikutana na uongozi wa Polisi pamoja na Meya wa Los Angeles Eric Garcetti.

The Game amesema ameguswa kufanya hivyo sababu ameona hali inavyoelekea ni kwamba Ubinaadamu unaondoka ndio maana akaamua kutumia ushawishi wake kusaidia kumaliza au kukiondoa kinachotaka kutokea, sisi sio Wanyama.

snoop 3

snoop 4

H.U.N.T the movement !!! #HATEUSNOTTODAY #HUNTUSNOTTODAY

A video posted by The Game (@losangelesconfidential) on

ULIIKOSA HII YA MTANZANIA MAYUNGA NYUMBANI KWA AKON MAREKANI? BONYEZA PLAY KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments