AyoTV

VIDEO: Waathirika wa dawa za kulevya wapewa elimu ya ujasiriamali

on

Shirika la Global Sharpers linaloongozwa na vijana wenye elimu mbalimbali limetoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana zaidi ya 40 walioathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya waliopo kwenye nyumba maalum ya malezi.

Ayo TV na millardayo.com imetembelea South Beach Sober House iliyopo Vijibweni katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam ambako Global Shapers ilikuwa inatoa mafunzo ya ujasiriamali ili kuwafanya vijana hao kujiajiri baada ya kumaliza matibabu.

Inadaiwa kuwa watu ambao wameathiriwa na Dawa za kulevya bado wanatengwa na jamii hata pale wanapotoka kwenye nyumba za malezi wakidhaniwa kuwa bado hawajarekebika kutokana na matatizo yaliyopita.

Bonyeza play kwenye hii video kutazama…

Soma na hizi

Tupia Comments