Maajabu

Goli la Ronaldo lilivyomuamsha huyu mtoto alielala kwa miezi mitatu

on

Screen Shot 2014-04-08 at 9.56.42 PM

Ni mara nyingi tumesikia stori zinazomuhusu staa wa soka duniani Cristiano Ronaldo, zile zinazosisimua na zile zinazoleta furaha kwa kila shabiki wake…. ila hii inasisimua na kuleta furaha pia kuona kuna mtu alikua kwenye maumivu lakini yameondoka kutokana na Ronaldo.

Stori kutoka Poland ni kwamba goli la mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo lilimsaidia mtoto aliyepoteza fahamu kwa muda wa miezi mitatu kurudiwa na fahamu zake.

David Pawlaczyk (14) aligongwa na gari akiwa anaendesha baiskeli na kupata majeraha makubwa kichwani August mwaka jana, alipelekwa hosptali lakini akapoteza fahamu kama ilivyoripotiwa na gazeti la Poland la Fakt.

Ronaldo akiwa na familia ya David.

Ronaldo akiwa na familia ya David iliyosafiri kuitikia mwaliko uliotolewa na Ronaldo baada ya kusikia stori ya huyu mtoto.

Wazazi wake waliambiwa matibabu ya sauti ndio yalikuwa matibabu mazuri katika kumtibu hivyo wakapewa maelekezo kwamba wawe wanamuekea sauti ambayo atakuwa anaifahamu.

David alikuwa shabiki mkubwa Real Madrid na wazazi wake walimuwekea matangazo ya radio ya mechi za Real Madrid ikiwa ni moja ya mbinu za kujaribu kumtibu.

Screen Shot 2014-04-08 at 10.02.15 PMWakati Ronaldo alipofunga goli wakati wa mechi ya kogombea kucheza kombe la dunia dhidi ya Sweden David alikuwa akisikiliza matangazo ya mechi hiyo na baada ya goli la Ronaldo, mtoto huyo ndio akaamka ghafla.
article-2599601-1CECEFFD00000578-493_634x946Vyombo vya habari vya Poland viliripoti tukio hilo na likamfikia Ronaldo na mchezaji huyo akawaalika David na wazazi wake kwenda kuangalia mechi ya Real Madrid vs Dortmund.

Kwenye hii video hapa chini unaweza kutazama video ya jinsi mtoto huyu alivyoianza safari na wazazi wake mpaka kukutana na Ronaldo…. vilevile kumbuka kuungana na millardayo.com kwenye twitter, instagram na facebook kwa jina hilohilo la MillardAyo ili matukio kama haya yasikupite.

Tupia Comments