Najua umezoea kusikia zile headlines za wanamichezo kadhaa wakiingia katika shutuma za kutumia dawa za kuongeza nguvu michezoni dawa ambazo zimekatazwa kutumika katika michezo. Miongoni mwa wanamichezo ambao wamekuwa wakituhumiwa kutumia dawa hizo ni wanariadha na mabondia.
Stori zilizopo katika headlines kwa sasa zinamuhusu staa wa soka wa Brazil anayekipiga katika klabu ya Shaktar Donetsk ya Ukraine Frederico Rodrigues Santos ambaye amezoeleka kama Fred, amefungiwa na shirikisho la soka la America (CONMEBOL) baada ya kugundulika kutumia dawa za kuongeza nguvu ambazo zimekatazwa kutumiwa michezoni.
Fred anatajwa kugundulika kuwa katumia dawa aina ya Hydrochlorothiazide, hivyo amefungiwa na shirikisho hilo kuichezea timu ya taifa ya Brazil hadi June 27 2016. Staa huyo atakosa mechi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 Urusi. Michezo ya Brazil atatkayoikosa Fred ni mechi kati ya Brazil dhidi ya Paraguay na Uruguay. Fred anaingia katika headlines za Kolo Toure ambaye alifungiwa mwaka 2011 kwa tuhuma hizo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.