Michezo

Solskjaer aeleza mbinu anazotumia kuwafuatilia wachezaji wake kwa sasa

on

Siku chache ikiwa imepita baada ya kocha wa Tottenham Hotspurs Jose Mourinho atangaze kuwa ataanza mazoezi na wachezaji wake kwa njia ya video, leo kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer ameeleza mpango wake.

Solskjaer ameeleza kuwa licha ya kujitenga kwa wachezaji wake lakini amekuwa akiwasiliana nao mara kwa mara kuhakikisha kuwa wachezaji hao wanafuata program maalum na kuhakikisha wanatunza utimamu wa mwili.

“Nimekuwa nikiwafuatilia mwenendo wao kila siku na saa kwa saa, nimekuwa nikiwasiliana nao kwa kupitia group la whatsapp na jumbe za kawaida, tunapanga tutakaporudi ni aina gani ya mazoezi tutakuwa tukiyafanya lakini hatujui hata tutarudi lini”>>>Ole Gunnar Solskjaer

Soma na hizi

Tupia Comments