Kocha wa Manchester Utd Ole Gunnar Solskjaer amewasilisha salam za kuomba radhi kwa niaba wamiliki wa klabu hiyo Familia ya Glazer na amesema kuwa wamiliki hao wanawasikiliza sana mashabiki wa timu hiyo, licha ya kukaa kimya juu ya kuwepo kwa maandamano ya hasira toka kwao.
Solskjaer ameongeza kusema kuwa familia ya Glazer imemuomba msamaha yeye mwenyewe binafsi juu ya maamuzi yao ya kutaka kujiunga na European Super League.
Pia Ole amelaani vurugu zilizo sababisha kuahirishwa kwa mchezo wa Jumapili dhidi ya Liverpool, akisema kwamba waandamanaji walienda mbali zaidi hadi kusababisha vurugu hizo.
Vilevile amesisitiza kuwa wamiliki hao wa kimarekani wamejitolea kuboresha mawasiliano yao na mashabiki katika siku za usoni, licha ya Avram Glazer kukataa kuomba msamaha kwa wafuasi wa timu hiyo kwa kitendo cha kujaribu kujiunga na uropean Super League wakati alipotafutwa na waandishi wa habari nyumbani kwake Palm Beach Jumanne hii.