Nahodha Son Heung-min anasema anataka kukumbukwa kama gwiji wa Tottenham Hotspur, lakini haamini kuwa anaweza kuzingatiwa kuwa hivyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 anakaribia mwaka wake wa 10 katika klabu hiyo ya Ligi ya Premia na amewachezea zaidi ya mechi 500.
Amefunga angalau mabao 14 katika kila misimu minane iliyopita na akaanzisha ushirikiano mzuri na Harry Kane kabla ya nahodha huyo wa Uingereza kuhamia Bayern Munich majira ya joto yaliyopita.
Alipoulizwa ni historia gani ambayo siku moja angependa kuacha katika klabu hiyo, fowadi wa Korea Kusini Son aliiambia BBC Sport: “Legendary.
“Kuwa katika timu moja ndani ya miaka 10 ni juhudi nzuri nadhani.
“Bado sidhani kama mimi ni gwiji wa klabu hii. Nimesema nataka kushinda kitu nikiwa na Spurs, basi nataka kuwa na furaha sana kuitwa gwiji.
“Nilijiunga na Spurs kushinda kombe na ninatumai tunaweza kufanya msimu maalum.”
Tottenham hawajashinda taji lolote kubwa tangu Kombe la Ligi mwaka wa 2008, lakini Son anatumai kuwasaidia kutwaa ubingwa msimu huu, haweki malengo yoyote ya kibinafsi.
Msimu uliopita alifunga mabao 17 katika Premier League huku Spurs ikimaliza nafasi ya tano.
“Siweki lengo la mahali ninapopaswa kuwa,” alisema.